LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 17, 2016

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM LATOA TAMKO KUMUUNGA MKONO RAIS DK. JOHN MAGUFULI

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU CCM TANZANIA     

TAARIFA KWA UMMA

Katibu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu
 ya Juu-CCM, Siraji Madebe
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu CCM  katika kikao chake cha kazi cha Agosti 11, 2016, pamoja na mambo mengine. 
Kimeazimia yafuatayo:-

Kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuelimisha wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu umuhimu wa kila mwananchi kudai risiti na muuzaji kutoa risti katika kila manunuzi, kwa lengo la kuwezesha serikali kupata fedha kupitia kodi, kutoa elimu kwa jamii na uelewa wa Tanzania yenye viwanda ikiendana na uwanzishaji wa mashamba darasa ya shirikisho na viwanda vya kati vya kusindika mazao.

Vilevile Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, tunafungua milango kwa vijana mbali mbali wenye lengo la kuunda vikundi vyenye dhamira ya kujikwamua kiuchumi na kutaka kujiajili, kufika kwenye ofisi zetu za Shirikisho zilizopo mikoani na Makao Makuu, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, ili kupata ushauri wakitaalamu na kusaidiwa kuandika maandiko yatakayo waongoza kwenye uanzishwaji wa miradi itakayo saidia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Pia Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, linamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, kuwashughulikia kikamilifu wale wote waliohujumu mali za CCM, kwani vitendo hivyo vinadhoohofisha nguvu ya chama na wakati mwingine kuwafanya wanachama kuwa wanyonge kwenye Chama chao.

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, kwa kuhamia Dodoma, tumeazimia kuwa Ofisi ya Makao Makuu ya Shirikisho nayo itahamia Dodoma rasmi hivi karbuni, baada ya taratibu za upatikanaji wa Ofisi kukamiliaka.

Mwisho, Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, linapenda kuwaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono na kumuamini kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani dhamira yake ni kuitumikia jamii ya Watanzania na si kufanya siasa kwenye maisha ya watu wenye shida.

KUDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano
Shirikisho Makao Makuu

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages