Friday, August 26, 2016

SERIKALI YASEMA, MITIHANI YA DARASA LA NNE NA KIDATO CHA PILI BADO IPO, KUFANYIKA PIA MWAKA HUU

Dk. Leonard Akwilapo
Na Lilian Lundo - MAELEZO
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mitihani ya Taifa ya Darasa la nne na Kidato cha pili mwaka huu itafanyika kama kawaida.

Napenda niukumbushe Umma kuwa mitihani hii ya darasa la nne na kitado cha pili ni muhimu sana katika ufuatiliji wa maendeleo ya wanafunzi wetu. Kwa hiyo itaendelea kuwepo na mwaka huu itafanyika kama kawaida, na kama kuna watu wanawaambia kuwa haitafanyika wawapuuze kabisa,”.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard Akwilapo, akikanusha taarifa za uvumi unaoenezwa kuwa mitihani hiyo haitakuwepo kwa mwaka huu wa 2016.

Dk. Akwilapo alisema kuwa, mitihani hiyo ina umuhimu mkubwa katika kupima maendeleo ya mwanafunzi kwa lengo la kufanya maendeleo ya kitaaluma. Aidha kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajafikia viwango vya ufaulu vilivyowekwa watatakiwa kukariri darasa au kidato.

Amebainisha kuwa Baraza la Mitihani ndilo lenye jukumu la kushughulikia maandalizi ya mitihani hiyo ikiwa ni pamoja na utungaji, uchapaji, ufungaji na usafirishaji hadi ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) ikiwa na majukumu ya kuhakikisha kuwa uendeshaji na usahihishaji wa mitihani hiyo unafanyika kikamilifu.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.