Friday, August 19, 2016

RAIS DK. MAGUFULI AMUAPISHA LEO MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.
 . Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
------------------ 
TAARIFA KAMILI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Agosti, 2016 amemuapisha Bw. Mrisho Mashaka Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Mashaka Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Bwana Mrisho Mashaka Gambo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Daudi Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.