Wednesday, August 31, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) ASEMA WAZEE WA CHAMA HICHO NI ‘WAONGO’., 
Na Nassir Bakari 0713 311 300
Ile hali ya sintofahamu iliyoanza kujitokeza tangu tarehe 21/08/2016 kwenye ukumbi wa Blue Pearl , Ubungo Plaza, Dar es Salaam kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), imeendelea baada ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Nassor Ahmed Mazrui, kuwaita wazee wa chama hicho ‘waongo’ baada ya wazee hao kufanya mkutano na kusema Maalim Seif anakigawa chama.

Kauli hiyo imekuja siku moja, baada ya wazee wa chama hicho wa mkoa wa Dar es Salaam, kuitisha kikao na waandishi wa habari kilichoongozwa na  Katibu wa wazee wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Rajabu Magomba na kusema kuwa kuna mkakati wa makusudi unaofanywa na katibu mkuu, Maalim Seif Shariff Hamad wa kukiua chama hicho kwa upande wa Tanganyika.

Akijibu shutuma hizo Naibu katibu mkuu wa chama hicho, ndugu Nassor Ahmed Mazrui alisema yote yaliyozungumzwa na wazee hao, sio ya kweli  na hayana mashiko.
“Yote hayo ni uongo mtupu, Chama kikiwa cha upande mmoja kinafutwa na Msajili leo Maalim awe mjinga kiasi gani hata agawe Chama.”

Pia, katibu mkuu huyo aligusia swala la aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, kurejea kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho na kusema hata iweje chama cha wananchi(CUF), hakitoweza kumruhusu kurudi tena kwenye nafasi hiyo.

“Sasa utamrejesha mtu aliyejiuzulu ndugu yangu, mimi ningemshauri asubiri hadi mwaka 2018.”

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.