LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 14, 2016

MKURUGENZI MALINYI ATOA FURSA YA AJIRA KWA WAHITIMU ZAIDI YA 35 WA VYUO VIKUU

Marcelin Ndimbwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Malinyi mkoani Mrogoro, Marcelin Ndimbwa ametekeleza ahadi yake na kuunga mkono maagizo ya serikali kuondoa umasikini hasa kwa vijana kwa Halmashauri hiyo kuwapatia ekari 45 vijana zaidi 35 wahitimu 35 wa vyuo vikuu kwa ajili ya kilimo cha mpunga kwa njia ya skimu.

Akizungumza leo, Ndimbwa amesema pamoja na ekari 45 walizopewa, pia watapewa bure mbegu, na baada ya kupanda itawachukua siku 85 mavuno kuwa tayari ambapo mujibu wa msimamizi wa mradi huo Ofisa Kilimo, Mhandisi, Maimuna Makutika ekari moja lina uwezo wa kutoa magunia 40 hadi 50.

Fisa kilimo huyo ameongeza kwamba gharama ya kuhudumia ekari moja hadi kufikia hatua ya mavuno haizidi 600,000, huku gunia moja kwa wastani wa bei, mwezi Desemba hadi Janauari huzwa kwa sh 80,000 hadi 120,000, hivyo kwa wastani  ekari 45 zitatoa kiasi cha sh 180,000,000.

Mkurugenzi Ndimbwa amesema kupitia uwekezaji huo vijana watakua wamepata ajira ya kudumu na pia watakua wamejikwamua   kiuchumi  kama watafanya bidii na kuyatunza mashamba hayo inavyostahili.

Pia Mkurugenzi amesema kupitia mradi huu wa kilimo uchumi wa watu wa Malinyi utakua pamoja na kuhamasisha jamii  inayozunguka wilaya hiyo kujiajiri kwa kuwekeza katika Kilimo ili kujikwamua kutoka katika wimbi la umasikini na kuongza kuwa tayari vikundi vya vijana wilayani hapo vimehamasika baada ya kuona mwitikio wa wasomi kuwekeza kwenye kilimo ambapo hadi sasa vijana wenyeji walioitikia ni zaidi ya 150, vikundi 30 na ekari zaidi ya 200 zishalimwa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages