LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 28, 2016

JESHI LA POLISI LAONGEZA ASKARI 80 KATIKA OPERESHENI YA KUSAKA MAJAMBAZI VIKINDU, MKURANGA

 
Jeshi la Polisi wakiwa kwenye magariNa:Nassir Bakari
0713 311 300
Kufuatia mpambano mkali na majambazi,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeongeza nguvu kwa kutuma askari wengine 80 katika oparesheni ya kusaka majambazi inayoendelea katika maeneo ya Vikindu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na vyombo vya habari leo katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo Kamishna Simon Sirro, amesema Jeshi hilo limeanza rasmi oparesheni hiyo usiku wa kuamkia jana, ikiwa na lengo la kusaka watu wanaoshukiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kufanya matukio kadhaa ya ujambazi likiwemo lile la kuuawa kwa askari wanne waliokuwa wakienda lindoni, katika benk ya CRDB, Mbade jiji Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika oparesheni hiyo kuna watu waliouawa na wengine wanashikiliwa na jeshi hilo, lakini amekataa kutaja idadi yoyote ile ya waliouawa au waliokamatwa kwa sababu za kiusalama kwa kuwa oparesheni hiyo bado inaendelea.

“Itakuwa ni kinyume cha utaratibu nikieleza kinachoendelea kwenye operesheni, niwahakikishie silaha zilizochukuliwa zinarudi,kinachoendelea nitawajulisha jumanne ili wananchi wajue kitu gani kinaendelea,” amesema.

Ameongeza kuwa; “Mapambano ni ya kawaida sana, na ndio maana askari polisi akifa kwa silaha ni jambo la kawaida sana. Operesheni tutaifanya maeneo ya Vikindu, Pwani Dar es Salaam, sababu hii network (mtandao) ipo na lazima tutaisafisha.Kama walidhani wataitawala DSM wamejidanyanya lazima tutarudisha heshima ya jiji.”

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages