CHADEMA YAAHIRISHA OPERESHENI UKUTA


 Na Nassir Bakari 0713 311 300
 MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe mapema leo, ametangaza,  Chadema imeahirisha 'Operesheni UKUTA' hadi Oktoba Mosi kutoa nafasi ya mazungumzo kati ya Rais na viongozi wa Dini.
 
"Tunaahirisha mikutano, maandamano UKUTA kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka," alisema Mbowe.