Monday, August 15, 2016

CCM YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS WA AWAMU YA PILI WA SMZ MZEE ABOUD JUMBE MWINYI.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea jana tarehe 14th Agosti 2016 nyumbani kwake Mji Mwema, Kigamboni  jijini Dar es salaam.

Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Chama cha Mapinduzi mara baada ya kuunganisha Chama cha ASP na TANU.

Mzee Jumbe alikuwa ni Kiongozi mchapakazi, Muasisi na Mwanamapinduzi aliyeshiriki katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ametoa mchango mkubwa katika kuunganisha vyama vya TANU na ASP. Ameweka rekodi nzuri ya kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyetumikia nafasi hiyo kwa muda mrefu (1972 – 1984) na kutembelea Vijiji na Wilaya nyingi za Tanzania Bara na Zanzibar na kusikiliza kero na changamoto za wananchi.

Aidha, Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Ali Mohamed Shein, familia ya Mzee Aboud Jumbe pamoja na Wazanzibari wote kufuatia kifo cha Kiongozi wetu. Tunaungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu.


WanaCCM nchi nzima tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.  Amina

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.