BODI YA FILAMU TANZANIA YACHARUKA, YATOA SIKU SABA KWA KAMPUNI PAMOJA FILM KUWASILISHA NYAKA ZA KAZI ZAO

JOYCE FISSOO
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Bodi ya Filamu Tanzania imetoa siku saba kwa Kampuni ya Usambazaji wa Filamu ijulikanayo kama ‘Pamoja Film Company’ kuwasilisha nyaraka za filamu zake ili kuhakikisha kama wamefuata sheria na kanuni zinazosimamiwa na bodi hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kampuni hiyo kubainika kukiuka baadhi ya sheria na kanuni za usambazaji zikiwemo za kutowasilisha miswada ya filamu (script) kabla ya kuanza kurekodi, kuzitangaza kazi hizo kwenye mitandao ya kijamii bila ya kuzifikisha Bodi ya Filamu Tanzania Kwa ajili ya ukaguzi pamoja na kufanya kazi za utengenezaji na usambazaji wa filamu bila kibali.

Agizo hilo limetolewa leona Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo alipokutana na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Lufingo Exaud,  kwenye  kikao kilichofanyika ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa kukiuka sheria...Kusoma zaidi habari hii tafadhali >>>GONGA HAPA

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.