Saturday, August 27, 2016

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI NA MAJUKUMU YAKE

Msajili wa vyama Jaji Mutungi
Kumekuwa na changamoto  kwa baadhi ya Wananchi na vyombo vya habari na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu Baraza la vyama vya siasa hapa Tanzania, na majukumu yake kisheria.

Kufuatia hali hiyo, tumeona tutoe elimu japo kwa ufupi kuhusu Baraza hili, ili kutoa mwanga zaidi kwa wale ambao hawalifahamu Baraza hilo

Baraza la Vyama vya Siasa limeanzishwa chini ya kifungu cha 21B cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 ikiwa ni jukwaa la viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kukutana mara kwa mara kujadiliana masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi na siasa hapa nchini kwetu.
Kila chama cha siasa kinawakilishwa na viongozi wawili wa ngazi kitaifa katika Baraza la Vyama vya Siasa, ambapo kiongozi mmoja anapaswa kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar. Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti wa Baraza huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Baraza la Vyama vya linaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za zilizotungwa na Baraza.
Baraza la vyama vya siasa lina majukumu yafuatayo:-
1.    Kumshauri msajili wa vyama vya siasa kuhusu migogoro baina ya vyama vya siasa;
2.    Kumshauri Msajili wa vyama vya siasa kuhusu masuala yenye masilahi ya kitaifa yanayohusu vyama vya siasa na hali ya siasa nchini;
3.    Kuishauri Serikali kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu kutungwa, marekebisho na utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na sheria nyingine zinazohusu vyama vya siasa;
4.    Kushauri kuhusu uratibu wa shughuli za vyama vya siasa; na
5.    Kumtaarifu Msajili wa Vyama vya Siasa kuhusu masuala yoyote yanayohusu utendaji wa chama chochote cha siasa.
Kamati ya uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti wa Baraza, Makamu Mwenyekiti wa Baraza, wenyeviti wa kamati nne za Baraza na katibu wa Baraza.
 
English version
The Council of Political parties is the council established within the office of Registrar of political parties by the Political Parties Act Chapter 258. Its members are two national Leaders of each political party with full registration. The Chairman and Vice Chairman of the council are elected by the members of the council. The office of Registrar of political parties provides secretariat to the Council.

Functions of the Council of political parties are as follows:-
1.    Advices the registrar on the disputes arising amongst political parties;
2.    Advices the Registrar on matters of national interests with reference of political parties or political situation;
3.    Advices the government through the Registrar on enactment, amendment and implementation of political parties act and other laws relating to political parties;
4.    Advices of the regulations prescribing matters regarding political parties; and
5.    Inform the Registrar on any matter regarding the operation of any political party.

kwa ufafanuzi zaid  piga 0658717262
Monica Laurent
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.