LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 24, 2016

MSANII WOLPER ALIYEKUWA MPIGA DEBE WA LOWASSA 2015 ATIMKIA CCM

 Msanii Jacquiline Wolper (katikati) ambaye mwaka jana alikuwa mmoja wa wasanii wapiga debe wa aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, akikaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Jakaya Kikwete baqada ya kutangaza kujiunga na CCM akitokea Chadema juzi usiku wakati wasanii wakitumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma. (PICHA NA KAMANDA  RICHARD MWAIKENDA)
 Wolper akifurahi kujiunga CCM ambapo alisema anaomba asamehewe kwa kitendo chake cha kumpigia kampeni Lowassa mwaka jana
 Msanii Jacquiline Wolper akifurahi alipokuwa akikaribishwa na Mwenyekiti mstaafu, Jakaya Kikwete baada ya kutangaza kujiunga tena na CCM akitokea Chadema jana usiku wakati wasanii wakitumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Wolper akiwa na furaha ya wazi baada ya kukubaliwa kujiunga na CCM


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages