LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 4, 2016

POLISI WATAKIWA KWENDA NA WAKATI KWA KUTUMIA ZANA NA TEKNOLOJIA ZA KISASA-UN

Na Mwandishi Maalum, New York
Viongozi Wakuu  wa Polisi   kutoka  nchi  mia moja  ambazo  zinachangia  polisi wao  kuhudumu katika ulinzi  wa amani  na usalama kupitia Umoja wa Mataifa,  wamekamilisha  mkutano wao wa siku moja  uliofanyika jana Ijumaa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Huu ni  mkutano kwa kwanza wa aina yake kuwahi kufanyika,  ambapo wakuu wa  Polisi ( IGPs) wamekutana kwa wingi na kwa wakati mmoja tangu shughuli za  Kipolisi  zilipoingizwa katika  Operesheni za Ulinzi wa Amani kupitia  mwamvuli  wa Umoja wa Mataifa.

Katika mkutano huu na ambao washiriki walijadiliana, kubadilishana uzoefu, na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kubadilishana za   ulinzi na usalama katika nganzi  ya Kimataifa,  uliandaliwa na  Kitengo cha Polisi cha Umoja wa Mataifa ( UNPOL), kitengo ambacho ni sehemu ya Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa,  na   ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson.

Ujumbe wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania   ni kati ya nchi  ambayo  kwa miaka  kadhaa sasa imekuwa ikitoa  Polisi wake kushiriki katika  misheni za ulinzi wa Amani  chini ya Umoja wa Mataifa,  umeongozwa  na  Naibu Kamishna wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Maalum  Bw. Daniel Nyambabe.

Akizungumza kwa njia ya  video  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban   Ki Moon,  amesema. “ Kutoka  Kabul hadi Kishansa na kutoka  Port-au Prince  hadi  Pristina,  Polisi wa Umoja wa Mataifa wanatekeleza majukumu yao katika mazingira magumu, hatarishi   na yenye changamoto nyingi. Lakini pamoja na  changamoto hizo bado polisi hawa welevu na mashuja wameendelea kulinda  jamii,wanaleta  mabadiliko katika  maeneo  hayo  na mengine mengi  kwa kurejesha utawala wa sheria na kufungua njia za upatikanaji wa  usalama na maendeleo  endelevu

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu  wa UN, Jan Eliasson,  ambaye alikuwa mgeni  rasmi katika  mkutano  huo , amewaambia  viongozi hao wa Polisi kwamba, kutokana na  changamoto  nyingi na kubwa zinazohusu     Amani na usalama wa Kimataifa,  utekelezaji wa  majukumu ya Polisi na kipolisi  kuanzia wale wanaohudumu na kushiriki katika  operesheni za Umoja wa Mataifa,  na  polisi wote duniani kote unatakiwa kubadilika na kuwa wa kisasa zaidi.

Maeneo ambayo Polisi wanatakiwa kubadilika katika utekelezaji wa  majukumu yao ni  pamoja na kuwa na zana na vifaa vya kisasa, uwezo mkubwa na weledi wa hali  ya juu katika ukusanyaji  na uchambuzi wa taarifa za kiitelejensia,  uwezo  mkubwa wa kukabiliana  na  kwa wakati na mitandao  ya kihalifu ya kimataifa ukiwemo ugaidi.

“Kabla ya  kumaliza  hotuba yangu,  ningepeda kusisitiza mambo kadhaa ya msingi ambayo ninaamini mtakubaliana nami. Maafisa wetu ( Polisi) wanatakiwa wawe tayari wakati wowote, wanatakiwa kuwa na vifaa  na zana za kisasa za kazi , wanatakiwa wawe wanaopewa   mafunzo ya hali ya juu,  wanatakiwa wawe na uwezo wa kuwafundisha wengine, wanaopashwa kuwa na uwezo kuwa na  teknolojia za kisasa, wanatakiwa  wawe na fursa ya  kupata taarifa za kiitelejensia na kuzifanyia kazi ipasavyo,  uwezo wa kupata takwimu za uhalifu na vifaa vya kuzifanyia uchambuzi takwimu hizo” akasema Eliasson.

Katika  kusisitiza hayo, pia ameongeza na kutilia mkazo nafasi  na fursa ya  Polisi wanawake  ya kushiriki  kwa wingi katika misheni za kulinda Amani. Na kuongeza pia kwamba, maafisa wa polisi wanatakiwa pia wawe ni  viongozi wenye uzoefu mkubwa, na wanatakiwa kuwa tayari kusaidia katika vita dhidi ya  unyanyasaji wa kijinsia na  kingono.

 Viongozi wengine waliowazungumza wajumbe hao ni  pamoja na Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani  ( DPKO)  Bw. Herve Ladsous  pamoja na  Bw. Atul Khare Mkuu wa DFS
Baadhi ya  Mada zilizojadiliwa katika mkutano wa wakuu hao wa Polisi ni pamoja na  changamoto za uhalifu wa kimataifa na Operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa,  hali ya sasa na  ya baadaye kuhusu Polisi waohudumu katika  Umoja wa Mataifa   pengo,   fursa   nafasi   na  utaalamu wa Polisi katika Umoja wa Mataifa. Baadhi ya mada hizo  zilitolewa na  wataalam kutoka INTEPOL,


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages