LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 9, 2016

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA NHC


001 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua rasmi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam ambapo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ambayo wafanyakazi wake wanaifanya kwani ndiyo shirika pekee la Serikali linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na kuiletea heshima serikali, Waziri Mabula amewaambia wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na Menejimenti yake kuendelea na kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ili kuleta maendeleo zaidi nchini katika sekta ya nyumba.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
01Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki katikia makao makuu ya shirika hilo Apanga kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na kushoto ni Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC.
1Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu kulia na Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC kushoto wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
3Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo.
4Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akipitia nyaraka huku Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha ili kufungua rasmi mkutano huo.
5 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
6 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akisisitiza jambo wakai akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Naibu Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
7Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba wakifuatilia mkutano huo.
8Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
9Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiwa katika mkutano huo.
11 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
12 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
13 
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages