Monday, May 2, 2016

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ATUNUKU VYETI KWA WASHIRIKI WA KAMPENI YA SIKU 10 YA USAFI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA)iv class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Zoezi la utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na washiriki wa kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) muda mfupi mara baada ya kurejea. 
Baadhi ya Washiriki wa Kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadicky alipokuwa mgeni rasmi katika Hafla ya kutunuku vyeti kwa washiriki pamoja na wamiliki wa kampuni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika Hafla hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa akizungumza katika hafla hiyo baada ya kukaribishwa huku akiwasilisha ombi la zoezi kama hilo la usafi lielekezwe katika lango la kupandia mlima la Londros lilopo wilayani Siha.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo ambao wanajulikana kama Wagumu.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Mtango Mtahiko akizungumza juu ya mafanikio ya kampeni ya siku 10 ya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Mhandisi Aisha Amour akifuatilia shughuli hiyo ya kutunuku vyeti ilivyokuwa ikiendelea .
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Betrita Loibook akizungumza katika hafla hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Betrita Loibook akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akiliongoza kundi la watu waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya usafi muda mfupi baada ya kurejea kutoka katika kilele cha mlima huo.
Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo.
Washiriki wa zoezi la usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick huku wakionesha vyeti walivyotunukiwa baada ya kufanikisha zoezi hilo.
Washiriki wakifurahia vyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza jambo na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.