DC KINONDONI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA OFISINI KWAKE

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi Mufti akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir.
DC KINONDONI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA OFISINI KWAKE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi leo asubuhi ametembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abuubakar Zubeir ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam. Mkuu wa Wilaya na mufti wamezungumzia ushirikiano katika suala la kuhamasisha na kujenga ari miongoni mwa waumini kufanya kazi, kutunza mazingira, kulinda amani na utulivu, kuiombea nchi yetu, kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli pamoja na wasaidizi wake wote ili waweze kutimiza vema majukumu yao kwa taifa letu.
Mufti Mkuu wa Tanzania alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa uamuzi wake wa kumtembelea na kumuahidi ushirikiano mkubwa katika kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.