Saturday, April 2, 2016

ZAIDI YA WAFANYAKAZI 250 WA DAWASCO WAFANYA USAFI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI.Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco ) Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki zoezi la usafi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watumishi wa Dawasco.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiweka maji katika moja ya mashine inayotumika kuzibulia miundombinu ya maji taka ijulikanayo kama Jet Machine.
Wafanyakazi wa Dawasco wakijaribu kuweka sawa mpira wa kunyunyiza maji ili kuondoa vumbi wakati wakifanya usafi katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Wafanyakazi wa Dawasco  wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Afisa Mtendaji Mkuu Dawasco Mhandisi Cyprin Luhemeja akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi baada ya kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Wengine ni wafanyakazi wa Dawasco.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi ,Cyprian Luhemeja akitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala ,Raymond Mushi ambaye pia alikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Dawasco mara baada ya wafanyakazi wake kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkuu wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi akizungumza na wafanyakazi wa Dawasco mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitali hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco akizungumza na wanahabri mara baada ya kufanya zoezi la usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meneja wa Dawasco eneo la Magomeni Mhandisi Paschal Fumbuka akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitai ya Taifa ya Muhimbili.
Baadhi ya vitendea kazi vya Dawasco vikiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
 (0755659929)
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.