RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA LUCY KIBAKIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe 26 Aprili, 2016.