LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 29, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI KIKAO KAZI CHA MAKAMANDA WA POLISI, WANASHERIA WA SERIKALI WAFAWIDHI WA MIKOA NA WAKUU WA UPELELEZI WA MIKOA NA VIKOSI MKOANI DODOMA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali,  Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad  Yusuph Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.



Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya kufungua kikao kazi hicho.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua kikao kazi hicho.

Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.
.............................
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.
Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.
Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
"Oysterbay pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment  na Polisi wenu wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction  ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli
Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya mwendesha Mashitaka wa Serikali kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
"Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea  mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi" amesisitiza Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.
Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages