LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 10, 2016

MSEMAJI MKUU WA CCM, MJUMBE WA NEC, CHRISTOPHER OLE SENDEKA AANZA ZIARA MKOA WA MANYARA, ASEMA CCM INAMTETEA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KATIKA KUTUMBUA MAJIPU

 Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa huo leo.
 Msemaji wa CCM, Mjune wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara kuanza ziara ya kikazi mkoani huo leo
 Katibu wa CCM mkoa wa Manyara, Ndengaso Ndakubali akimkaribisha Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda alipowasili Ofisi ya CCm mkoa huo leo akifuatana na Msemaji Mkuu wa CCM Christopher ole Sendeka katika ziara ya kikazi leo
 Msemaji wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili ofisi ya CCM mkoa wa Manyara leo kuanza ziara ya kikazi 
 Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akifuatana na Katibu wa CCM mkoa wa Manyara Ndakubali, wakati akitoka katika Ofisi ya CCM mkoa huo, tayari kwenda Wilaya ya Babati kuhutubia mkutano wa habadhara leo
 Msafara wa Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Ole Sendeka ukienda Babati
 Msemaji wa CCM na Mjumbe wa NEC, Ole Sendea (kushoto), akilakiwa na kinamama wa Kata ya Bashneti alipowasili kuhutubia mkutano wa habadhara katika kata hiyo wilayani Babati leo.
 Shamrashamra za kumsindikiza Ole Sendeka kwenda meza kuu
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimia baadhi ya wananchi na viongozi wa CCM wilaya ya Babati baada ya kuwasili katika Kata ya Bashneti, kuhutubia mkutano wa hadhara leo.
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwasailimia waasisi wa Chama katika wilaya ya Babati alipowasili Kata ya Bashneti wilayani humo mkoani Manyara leo 
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwasailimia wananchi kwa kuwapungia mkono alipowasili Kata ya Bashneti wilayani humo mkoani Manyara leo 
 Katibu wa CCM wilaya ya Babati Vijijini, KhabasMwijuki akitoa maneno ya utanguliza baada ya Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka lipowasili Kata ya Bashneti wilayani humo mkoani Manyara leo 
 Baadhi ya waasisi wa TANU na baadaye CCM wakiwa kwenye mkutano wa Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka uliofanyika  Kata ya Bashneti wilayani humo mkoani Manyara
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akivishwa vazi la wazee wa Kabila la wairaq, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Bashneti wilayani Babati mkoani Manyara leo
 Kina mkereketwa akiwa na picha ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere kwenye mkutano hu wa Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka katika Kata ya Bashneti wilayani Babati nmkoani Manyara leo 
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akiwa na wazee wa kimila ya kabila la Iraq, kabla ya kuhutibia mkutano wa hadhara katika kata ya Bashneti wilayani Babati mkoani Manyara leo 
 Kina mama wakiwa katika shangwe wakati wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kata ya Bashneti 

 Mzee wa kimila akiombea dua ya kimila mktano huo wa hadhara 
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Bashneti Beda Lukoa akimkaribisha Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC Christopher Ole Sendeka kwenye mkutano huo
 Diwani wa Kata ya Bashneti Jovita Mandoo akieleza mikakati ya Kata hiyo iliyopangwa kuleta maendeleo
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC< Christopher Ole Sendeka akiperuzi ilani ya CCM, kabla ya kupanda jukwaani kuhutubia mkutano wa hadhara. 
 Msemaji Mkuu wa CCM na Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akisalimiana na Karoli Oli, aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TANU kata ya Bashnet tangu mwaka 1962, baada ya kutambukishwa kwake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo 
 Katibu wa CCM mkoa wa Manyara akiendelea na utaratibu jukwaani kabla ya Ole Sendeka kuhutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Bashneti
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wialaya ya Mbulu mkoani Manyara, akimsalimia Msemaji Mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wakati wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kata ya Bashneti. Kulia ni Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda aliyeko katika ziara hiyo ya Msemaji Mkuu wa CCM.

 Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda akifungua pazia kwa kutoa hotuba fupi, kabla ya Msemaji Mkuu wa CCM, Chrstopher Ole Sendeka kuhutubia mkutano huo wa hadhara uliofanyika kata ya Bashneti, Babati mkoani Manyara leo
Msemaji Mkuu wa CCM, Mjumbe wa NEC, Christopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kata ya Bashneti, wilayani Babati mkoani Manyara leo.
    Sendeka, amesema, Chama Cha Mapinduzi kinamuunga mkono na kumtetea kwa nguvu zake zote Rais Dk. John Magufuli katika jitihada zake za kuliinua taifa la Tanzania.
      Amesema, CCM itafanya hivyo kwa sababu kazi anayofanya ya kupambana na wazembe na wezi wa mapato kwenye vyanzo vya uchumi wa taifa inatokana na maelekezo ya ilani ya CCM.
      Sendeka amesema, CCM inawataka wale wote wanaojaribu kupotosha jitihada zinazofanywa na Rais za 'kupasua majipu', kuwa ni kuwaone wanaochukuliwa hatia, kuacha mara moja, kwa sababu kinachofanyika ni sahihi na kwa mujibu wa sheria.
       Amesema, upasuaji majipu huo unaofanaywa na Rais Magufuli hauchagui bali yeyote anayebainika kuwa ni jipu hata akiwa mwana CCM haachwi.
       Kwa upande wake, Mjumbe wa NEC, Kilumbe Ng'enda, amewataka Watazania kutambua kuwa Uchaguzi umeshamalizika kwa hivyo asitokee yeyote kuanza kuweweseka, kwa kutoa maneno ya kejeli kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kwa sababu baada ya uchaguzi kumalizika sasa kiichobaki ni kuchapa kazi.
        Amsema, hakuna sababu za mwanasiasa yeyote kuanza mambo ya fitina za kisiasa wakati huu kwa kuwa kufanya hivyo anajisumbua.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages