Wednesday, April 27, 2016

DC HAPI AKAGUA MIRADI YA MWENGE


 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Salum Hapi akikagua miradi mbali mbali itakayozinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru katika kata zilizopo wilaya ya Kinondoni.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi jana tarehe 26/4/2015 alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoko manispaa ya Kinondoni. Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni, Mh. Hapi alikagua na kupokea taarifa ya miradi mbalimbali iliyokamilika na inayoendelea kukamilika. Miradi iliyotembelewa ni kama vile
-Mradi wa ujenzi wa soko la kisasa Mburahati utakaogharimu Bilioni 1.8,
-Mradi wa ujenzi wa barabara ya Arsenal Magoti uliogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1,
-Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Ubungo uliogharimu shilingi milioni 50,
-Ujenzi wa hostel ya wasichana katika shule ya sekondari Mabwepande utakaogharimu shilingi 283,988,270,
-Ujenzi wa Kalavati Mabwepande utakaogharimu shilingi 320,880,400,
-Ujenzi wa Kituo cha Kilimo Malolo Mabwepande utakaogharimu shilingi 96,412,200 na
-Ujenzi wa kisima cha maji Makongo utakaogharimu  shilingi 240,000,000.

Akiwa katika mradi wa Kilimo Mabwepande, Mh. Mkuu wa Wilaya alivutiwa na mradi huo ambao unalenga kuweka programu ya kuwafundisha wananchi kulima mbogamboga, kufuga kuku, samaki na ng'ombe. Mh. Hapi alitoa agizo kwa Mkurugenzi kuhakikisha fedha zilizosalia kulipwa mkandarasi kiasi cha shilingi milioni 30 zilipwe haraka ili kituo kikamilike, jambo ambalo lilikubaliwa palepale.

Miradi ya maendeleo iliyokaguliwa inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kuwa Kinondoni katikati ya mwezi ujao.

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.