Monday, March 7, 2016

WANA TABORA WANAOISHI DAR WAPATA UONGOZI

 Ndugu Imani Matabula akiomba kura kwa wajumbe
 Ndugu Imani Matabula akipiga kura yake wakati wa uchaguzi huo.
Ndugu Imani Matabula akila kiapo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo mbele ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Rukia Thabit.

Umoja wa wana Tabora waishio Dar es Salaam kupitia jumuiya ya Tabora Kwanza  jana tarehe 6 Machi wamefanya uchaguzi wa kwanza rasmi tangu jumuiya hii kusajiliwa na kumchagua Ndugu Imani Matabula kuwa Mwenyekiti wao kwa kipindi cha miaka minne kwa mujibu wa katiba. Jumuiya hii inajumuisha wilaya zote za Mkoa wa Tabora yaani Tabora Manispaa,Uyui,Sikonge,Urambo,Kaliua,Nzega na Igunga
Wajumbe waliohudhuria  kilichofanyika kwenye hotel ya Lamada jijini Dar es salaam walikuwa 27 kati ya 32. Inahusisha waliozaliwa,kusomea,kuishi au kufanya kazi katika Mkoa wa Tabora na wale wenye mapenzi mema na Mkoa wetu wa Tabora. Karibuni tushirikiane. Umoja huo pia ulimchagua Jannat Mzee kuwa Makamu M wenyekiti na Idrisa Mangapi kuwa Mweka Hazina.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.