LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 31, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


                              Msemaji wa CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka
Kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.

Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.
Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi, dini wala kabila, na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.
CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.
Chama Cha Mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Ndugu Christopher Ole Sendeka   
MSEMAJI WA CCM 
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
31/03/2016

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages