Thursday, March 31, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (BARA), RAJABU LUHWAVI AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA CCM MKOA WA MBEYA LEO, AWATAKA KWENDA NA KASI YA MABADILIKO YA CHAMA

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi hiyo, akiwa katika ziara ya kikazi leo. Anayemsalimia ni Katibu wa CCM wilaya ya Mbarali Abdallah Mpokwa.  Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo Mwangi Kundya
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia ni Katibu ambaye hajapangiwa kituo, Mariam Yusuf
 Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya akimsindikiza Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Bara Rajab Luhwavi kwenda ukumbini kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya CCM mkoa huo leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi katika Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya leo. Kulia kwake ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rajabu Luhwavi akiwasili ukumbini
 Katibu wa UVCCM mkoa wa Mbeya Adiya Mamu akihamasisha watumishi wa Chama, kumkaribisha ukumbini Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Rajabu Luhwavi leo
 Watumishi wa CCM Ofisi ya CCM mkoa wa Mbeya wakiwa ukumbini
 Katibu wa CCM, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Lobe Zongo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Bara kuzungumza na wafanyakazi hao wa Chama mkoa wa Mbeya
 Watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara alipozungumza nao
 Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Mwangi Kundya akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi kuzungumza na watumishi wa Chama mkoa huo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akizungumza na watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akizungumza na watumishi wa Chama mkoa wa Mbeya. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO>Picha zaidi>>BOFYA HAPA

Na Bashir Nkoromo, Mbeya
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( Bara) Rajab Luhwavi, amewataka watumishi wa chama kubadilika kwa vitendo ili kwendana na hali ya mazingira yaliyopo sasa na kuonya kuwa asiyetaka kwendana na mabadiliko hayo ataachwa kupisha wengine waendelee.

Amesema, mabadiliko ndani ya CCM, siyo dhana iliiyoanzishwa wakati wa uchaguzi mkuu, kama vilivyojinadi baadhi ya vyama wakati huo, bali ni dhana ambavyo Chama kiliiazimia kuitekeleza wakati wa mkutano wake mkuu uliopita.

Luhwavi alisema hayo, leo mjini Mbeya wakati wa kikao chake na wafanyakazi wa Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake katika mkoa huo, kikao ambacho pia alikitumia kuwapa fursa watumishi wa kada mbalimbali kuelezea kero au changamoto zote zinazowakabili kama wafanyakazi wa chama.

Luhwavi alisema ni lazima kila mtumishi wa chaa kuwa mstari wa mbele kwa kufayakazi kulingana na wakati uliopo ili ifikapo mwaka 2020 wananchi waikubali CCM kutokana na kile kilichofanyika.

Alisema, watumishi wa CCM, ndiyo nguzo muhimu ya Chama katika kila jambo, akifafanua kwamba watumishi wa Chama ni tofauti na viongozi wa chama kwa kuwa viongozi wao si watendaji bali ni watekelezaji wa yale anayokuwa wameandaliwa na watumishi.

"Ninyi ndio mnaosababisha picha halisi ya Chama ionekane vipi, siyo viongozi, maana ninyi ndio ambao huandaa hata
mikutano ya viongozi, na ili mikutano hiyo ionekane imefaa ninyi nndiyo chachu, kwa hiyo watumishi ndiyo nguzo kubwa ya Chama katika ufanisi wake", alisema Luhwavi.

Mapema, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya Alhaji Mwangi Kundya alimpongeza Naibu Katibu Mkuu kwa hatua yake ya kuamua kuzungumza na watumishi wa chama, na kwamba katika utumishi wake ndani ya Chama hiyo ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuhudhuria kikao ambacho Naibu Katibu Mkuu anazungumza na wafanyakazi.

Kundya alimuomba Naibu Katibu Mkuu kuwapangia vituo vya kazi makatibu watatu, ambao wapo kwenye Ofisi ya CCM ya 

mkoa huo huku wakiwa hawana kazi maalum.

"Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, tunao Makatibu watatu hapa, lakini hawajapangiwa vituo, sasa tutakuwa tunaendelea kuwalipa huku hakuna kazi wanazofanya, mwisho tutaonekana na sisi ni majipu, maana kazi zilizopo hapa si nyingi kiasi cha kuhitaji makatibu hao wa nyongeza", alisema  Kundya.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Luhwavi yupo katika ziara ya kukagua uhai wa Chama ndani ya Chama katika mkoa huu wa Mbeya, kabla ya kwenda Njombe.Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.