Wednesday, March 9, 2016

KIKAO CHA KWANZA CHA BODI YA BARABARA MKOA WA LINDI CHAFANYIKA LEO

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Jordan Rugimbana akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Kwanza cha Bodi ya Barabara kilichofanyika leo tarehe 9 Machi 2016 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,wengine waliokaa kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye na Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara ,Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali.

 Wajumbe wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani Lindi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Kikao Mhe. Jordan Rugimbana.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara mkoani Lindi.

 Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara ,Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali akijitambulisha kwa wajumbe wa kikao.
 Wajumbe wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani Lindi.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara mkoani humo.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akitaniana na Mwandishi maarufu wa mkoa wa Lindi Abdul Aziz


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Seleman Said Bungara almaarufu Bwege muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha Bodi ya Barabara cha mkoa wa Lindi.


Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.