Friday, February 26, 2016

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KUDAN KUSINI RIEK MACHAR, MJINI ADDIS ABABA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu wa Rais wa Sudani Kusini Riek Machar mjini Addis Ababa, Ethiopia mwishoni Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Chanjo.
      Katika mazungumzo hayo, Makamu huyo wa Rais alimshukuru Rais Mstaafu Kikwete kwa mchango ambao CCM imeutoa katika kusuluhisha mgogoro ndani ya chama tawala cha SPLM hadi  kufikiwa kwa makubaliano ya Arusha.  Ametumia pia fursa hiyo kuomba CCM kuendelea kukisaidia chama cha SPLM kutokana na uzoefu na ukomavu wake wa uongozi.
    Amemhakikishia Rais Mstaafu Kikwete juu ya azma yake ya kurejea Juba mapema iwezekanavyo.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete amempongeza kwa utayari wake wa kurejea Juba na amemuhakikishia kuwa CCM haitatupa mkono SPLM na itaendelea kushirikiana na kutoa mchango wake pale utakapohitajika. 
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.