LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 19, 2016

FASTJET WAOMBOLEZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA, MHANDISI SULEIMAN S. SULEIMAN

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi  Suleiman S. Suleiman.  


SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Dar es Salaam, 19 Januari, 2016

Uongozi na wafanyakazi wa Fastjet Tanzania  umepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa za  kifo cha ghafla cha Mkurugenzi Mkuu wa  wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi  Suleiman S. Suleiman.

Tunaungana na familia, marafiki, ndugu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kutuma salamu za rambirambi katika kipindi hiki cha kuomboleza.

Fastjet Tanzania imefanyakazi kwa ukaribu na Mhandisi Suleiman na tunatambua mchango wake katika kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.

Tutaukosa kwa kiwango kikubwa ushauri, uongozi na ushauri wake kutokana na kifo chake.

Tunaomba roho yake ipumzike kwa amani peponi.

Amin.


Imetolewa na Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages