Wednesday, January 13, 2016

CCM YATOA RATIBA YA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWAKE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongea na Waandishi wa habari kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama Cha Mapinduzi kila mwaka huadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Februari 05, 1977.  Mwaka huu kitakuwa kinatimiza miaka 39.

  1. UZINDUZI
Uzinduzi wa maadhimisho ya kumbukumbu ya hiyo utafanyika tarehe 31 Januari, 2016 Unguja, Zanzibar ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein.

  1. KILELE CHA SHEREHE
Kilele cha maadhimisho hayo Februari 06, 2016 mjini Singida ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dokta Jakaya Mrisho Kikwete. 

Viongozi wa kitaifa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria watapangiwa shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa kwa ujumla katika wilaya zote za mkoa wa Singida siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho hayo.

Mikoa yote iandae shughuli mahsusi kwa wiki nzima ya maadhimisho hayo, mkazo ukiwa ni kufanya shughuli za ujenzi wa Chama na Taifa katika maeneo yao, Mambo ya kuzingatia katika wiki hiyo ni kama ifuatavyo:-

i.             Kuingiza wanachama wapya wa CCM na Jumuiya zake na kufanya shughuli nyingine za kuimarisha Chama.
ii.            Kufanya mikutano ya kuwashukuru wana CCM na wananchi kwa kuiamini CCM kuendelea kuongoza Nchi yetu kwa kushiriki na kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo CCM ilipata ushindi wa kishindo wa Rais, Wabunge na Madiwani.
iii.           Kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo yao binafsi na ya Taifa.
iv.           Kushiriki shughuli za maendeleo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, upandaji miti, uchimbaji wa mitaro ya maji, kufanya usafi wa mazingira pamoja na shughuli nyingine za kijamii.

  1. KAULIMBIU
Kaulimbiu ya sherehe hizo ni “Sasa Kazi, Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.


Nape Moses Nnauye (Mb.),    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
13/01/2016
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.