LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2015

LAPF YATOA MSAADA WENYE THAMANI YA TSH 2,800,000/= KWA KITUO CHA AFYA MAKOLE DODOMA

Na Mwandishi Maalum
Mfuko wa Pensheni wa LAPF wenye makao yake makuu mjini Dodoma, umetoa msaada wenye thamani ya shilingi 2,800,000/= kwa kituo cha Afya cha Makole. Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni Mashuka 50, Vyandarua 50 pamoja na Vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwenye kituo hicho.

Msaada huo umelenga kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo wengi wao wakiwa ni kina mama wajawazito na watoto. LAPF inaunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za Afya nchini. 

Kadhalika katika kuadhimisha siku ya Uhuru tarehe 9 Disemba na kuunga mkono agizo la mheshimiwa Raisi Dk. John Pombe Magufuli la kufanya  usafi katika kuadhimisha siku  hiyo watumishi wa LAPF wakiongozwa na Mkurugenzi mkuu Bw. Eliud Sanga wameshiriki kufanya usafi katika maeneo yote ya nje na ndani ya kituo hicho  cha Afya cha Makole.

Mfuko wa Pensheni wa LAPF umekuwa ukitoa misaada mbali mbali ya kijamii nchini katika kuboresha huduma za kijamii kama elimu, maji, michezo, vituo vya kulea watoto yatima na afya. Katika sekta ya afya LAPF imekuwa ikitoa vifaa mbali mbali kama vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, dawa, mashuka, vyandarua pamoja kufanya ukarabati katika baadhi ya vituo vya afya kila bajeti ya misaada kwa jamii inaporuhusu.

LAPF inaamini kuwa misaada hii inawasaidia wanachama wake pamoja na watanzania wote kwa ujumla, pia inawaasa wadau wengine nchini kuchangia huduma mbali mbali za kijamii ili kuboresha maisha ya watanzania na hatimaye kuleta usawa katika jamii.

STAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
    
 Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akishiriki kufanya usafi katika maeneo ya kuzunguka ofisi za LAPF Dodoma pamoja na kituo cha Afya Makole.
 Baadhi ya Watumishi wa LAPF walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika kituo cha Afya Makole Dodoma Mjini katika kuadhimisha siku ya Uhuru.
 Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akizungumza jambo kabla ya kabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
 Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa Mashuka na Vyandarua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga akikabidhi Msaada wa vyandalua kwa ajili ya kituo cha Afya Makole kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dr. Jasmine Tisekwa.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akitoa shukurani kwa niaba ya uongozi wa kituo cha Afya Makole baada ya kupokea masaada. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages