Tuesday, October 6, 2015

MAGUFULI ALITIKISA JIJI LA ARUSHA MKUTANO WAKE WA KAMPENI WAVUNJA REKODI

 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha tayari kuhutubia wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa kampeni za CCM ikiwa Arusha ni mkoa wake wa 21 tangia kuanza kwa kampeni.
 Umati wa wakazi wa Arusha mjini ulivyofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kumsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Arusha mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapoa aliwaambia kuwa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atajenga Tanzania mpya yenye uchumi wa viwanda, ataondoa kodi ndogo ndogo ,wanafunzi kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne watasoma bure bila kulipa ada ya shule, ataboresha huduma za afya, miundo mbinu pamoja na kuboresha mahusiano na nchi jirani.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Arusha ambapo aliwaambia wakazi wa jiji hilo kuwa atakuwa Rais wa Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao wala dini na kabila.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa jiji la Arusha waliofurika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka akihutubia wakazi wa jiji la Arusha kwenye mkutano wa Kampeni za kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ambapo aliwaambia wananchi wa Arusha kuwa makini na siasa zinazolenga kutugawa kama Taifa.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa jiji la Arusha ambao leo wameweka rekodi ya kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya Tanzania, Magufuli na Amani wakati wa kufunga mkutano wa kampeni za CCM ambazo ziliongozwa na Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Arusha wakiimba wimbo maalum pamoja na Mastaa wa Muziki wa kizazi kipya.

 Yamoto Band wakitumbuiza mara baada ya mkutano kumalizika wa kumnadi Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Arusha mjini mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ,jijini Arusha.
 Kila bango lilibeba ujumbe.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli Namelok Sokoine kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Mto wa Mbu, Arusha.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mto wa Mbu Arusha kwenye mkutano wa kampeni za CCM, kulia ni mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Namelok Sokoine.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakazi wa Mto wa Mbu, Arusha.

 

 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani Marehemu Edward Moringe Sokoine , Monduli Juu.
 Wananchi wa Monduli wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa katikati ya wakazi wa Monduli.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Monduli ambapo aliwaambia wananchi wa eneo hilo kuwa atafanya kazi nao kwa heshima kubwa kama alivyofanya kazi Waziri Mkuu wa zamani Marehemu Edward Moringe Sokoine.
 Wakazi wa Monduli wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Monduli.
 Mgombea ubunge wa jimbo la Monduli Namelok Sokoine akihutubia wakazi wa Monduli kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa makuyuni waliojitokeza kwa wingi kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Longido.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Longido mkoani Arusha kwenye mkutano wa kampeni za kuinadi CCM pamoja na Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Longido mkoani Arusha kwenye mkutano wa kampeni za CCM.Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.