Saturday, October 24, 2015

MAGUFULI AFUNGA KAZI MWANZA

 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba tayari kuhutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM jijini Mwanza.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo amehitimisha kampeni zake jijini Mwanza ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria.
Katika mkutano huo wa kampeni  za aina yake zimehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mgombea mwenza wa urais Samia Suluhu Hassan
Akizungumza katika mkutano huo Dk. Magufuli amesema katika utawala wake taanza kutatua kero ya maji mijini na vijiji kwani tataizo hilo ameliona  katika kila eneo alilopita.
Amesema pamoja na kwenda katika mikoa yote lakini ameshindwa kufika kwenye majimbo matano ambapo ameahidi baada ya kuchaguliwa atakwenda kuwashukuru.
Naye Rais Kikwete, alimwagia sifa Dk. Magufuli na kusema kuwa ana sifa na vigezo vyote vya kuliongoza  Taifa na watu wake.
“Magufuli ni mwaminifu na mwadilifu ninawaomba Watanzania mumchague kwa kura nyingi,” amesema Rais Kikwete

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tayari kwa mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe akicheza muziki pamoja na Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Timu Bajaj wakitoa somo la kupiga kura.
 Msanii Fid Q akitumbuiza kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
 Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM. Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe akihutubia mbele ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu kwenye mkutano wa mwisho uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mgombea Mwenza Mama Samia Hasan Suluhu akihutubia wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa mwisho wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.