Saturday, October 10, 2015

KINANA AENDELEZA KAMPENI ZA NGUVU MKOANI KIGOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi Katanga,Kasulu mkoani Kigoma tayari kunadi sera za CCM kwa mwaka 2015-2020.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya shule ya msingi Katanga, Kasulu,mkoani Kigoma.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole akiomba kura kwa wakazi wa Kasulu Kusini mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Katanga.
 Mgombea ubunge wa Jimbo la Kasulu mjini Ndugu Daniel Nswanzigwanko akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kasulu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kasulu mjini.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi Kasulu mjini na kuwaeleza kuwa CCM imeleta mgombea anayejali wananchi, mtendaji na mfuatiliaji asiyependa rushwa na anatanguliza maslahi ya nchi kwanza kwa manufaa ya wote.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.