HABARI MPYA

Your Ad Spot

Oct 23, 2015

ASANTENI WAKAZI WA DAR

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia  wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikweteakimnadi mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani Dar es Salaam.
 Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam. 


Na Mwandishi Wetu.
Hakuna haikuwa rahisi kusogeza mguuu wala kusogea eneo moja kwenda jingine kutokana na idadi ya watu waliofurika kumshuhudia Dk.Magufuli ambaye anagombea urais huku Mwenyekiti wa ccm taifa Rais Jayaka Kikwete akisema tayari mgombea wao ameshinda urais.
Mkutano wa kumuombea kura Dk.Magufuli ulifanyika Dar es Salaam jana ambao sauti za watu zilizosikika kwenye eneo hilo walisikika wakiimba Dk.Magufuli rais na rais kikwete akieleza wazi Rais wa awamu ya tano ni Magufuli.
Kikwete amuita Magufuli Rais
Akizungunza mbele ya maelfu ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam , Rais kikwete alisema Rais wa awamu ya tano ni Dk.Magufuli na kuongeza sifa zake huwezi kufananisha wagombea wa vyama vingine.
Rais Kikwete alisema Rais ni Magufuli na wengine ni vivuli vya urais na kuwahakikishia watanzania kuwa hana mashaka hata kidogo baada ya uchaguzi mkuu kufanyika kesho kinachofuata ni kuapishwa kwa mgombea urais wa CCM.
Alisema Dk.Magufuli amezunguka nchi nzima kwa gari  na kote alikopita amehutubia wananchi zaidi ya saa moja na kueleza yale  ambayo ametumwa na chama wakati kuna mgombea ametumia helikopta lakini wameshindwa kuhutubia.
Alisema wakati Dk.Magufuli anazunguzia kila mahali na wananchi mgombea wa Chadema anashindwa kueleza sera  na kuwambia wananchi wakasome kwenye web site (mitandaoni).
"  unawaambia watu wakasome kwenye website na watu wanajiuliza hiyo website iko wapi.mgombea urais kwenye sifa ni Dk.Magufuli tu na hao wengine ni vivuli vya urais. Dk.Magufuli anawapenda vijana na mgombea pekee aliyezungumzia kupambana na rushwa.
*Mgombea yule mwingine hana sifa ya kuzungumzia rushwa na ufisadi kwani hana uwezo wa kupambana nayo.zaidi rushwa na ufisadi utastawi na kwa Magufuli rushwa itadhibitiwa na ndio maana anaeleza kutoka moyoni namna ambavyo atakabiliana nayo ikiwa pamoja na kuanzisha mahakama ya wazi.
Rais Kikwete alisema Dk.Magufuli anakubalika kutokana na sifa mbalimbali alizonazo ikiwemo ya uadilifu na utumishi uliotukuka na kuongeza Mgombea urais wa CCM ametimia kwa sifa na anatosha kwa kila upande na huyo ndio John Magufuli anayemjua yeye na ndio maana Ccm ilimchagua.
Alisema Magufuli kwenye kipindi cha kampeni amezungumzia namna ambavyo ameweka mipango ya kuongeza soko la ajira huku akijikita katika kueleza namna ambavyo atasimamia haki kwa watu wote.
"Magufuli ndio Rais sahihi wa awamu ya tano ,ameelezea makundi mengi atakavyoyatumikia na kuongeza Magufuli amesema namna atakavyowezesha wanawake kujishughulisha na uamendeleo yao na kuongeza kuwa ameahidi kuongeza fedha kwenye benki ya wanawake.
" Hivi kwa akina mama mna mtu Kama Magufuli mnahangaika na hao wengine wanini? Wakazi gani? Mpeni kura Magufuli awatumikie.Mtu wa aina ya Magufuli unamuachaje kumpa kura.
"Wenzetu wale hata siku moja hawajahi kuzungumza namna ambavyo atasaidia kundi la walemavu bali wao wanazungumzia kumtoa babu seya. kwa Magufuli ameeleza namna ambavyo atasaidia kundi la walemavu," alisema.
Rais Kikwete alisema Dk.Magufuli ameishi maisha ya watu masikini na anatoka familia ya wakulima na wafugaji hivyo ni atashughulia  maisha ambayo ameyaishi.
Amchambua Kingunge
Rais Kikwete alisema kuwa kuna  ametoka CCM akidai utaratibu wa kumpata mgombea urais wa CCM bali kilichotokea mzee huyo aliyemtaka hakupita.
Alisema utaratibu uliofanyika mwaka 1995 ndio ambao umetumika mwaka huu wa 2015 na kuongeza mzee (Kingunge ngambare mwiru) alikuwa na mtu wake hakupita na ndio sahihi anahaha kumtetea.
"Kuna mzee anazunguka na kudai utaratibu umekosewa si kweli .Mwaka 1995 Kingunge alikuwepo wakati huo huo na kilichotokea  utaratibu uliotumika wakati ile ndio huo huo," alisema Rais Kikwete.
Alisema kuwa hao ambao wapo upande wa pili wamekosa hoja na sasa wanahangaika na hata wengine kuzungusha mikono wanashindwa huku akiomba watanzania kumchagua Dk.Magufuli awe Rais wa awamu ya tano.
Azungumzia amani siku ya uchaguzi
Wakati huo huo, Rais Kikwete alisema kuwa siku ya uchaguzi mkuu utakuwa wa amani kwani serikali imejipanga vema na hakuna mahala ambapo kutatokea vurugu.
Pia alisema upinzani ulikuwa imekwend mahakamani kwa ajili ya kutaka wakae mita 200 kwa kigezo cha kulinda kura na kilichotokea walikwenda mahakamani na hatimaye wameshindwa.
Magufuli  na urais
Kwa upande wake mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli alisema kuwa amezunguka kwenye kampeni kwa gari ambapo ametembea zaidi ya kilometa 46000 na kote huko wanasema Rais ni Magufuli hivyo anaamini baada ya jumapili Rais atakuwa yeye.
Dk.Magufuli alisema atakuwa Rais wa watanzania wote na ndio maana baada ya kuanza ziara ya mkoa w Dar es Salaam alipokelewa na vyama vyote ikiwa pamoja na kuweka bendera mpya Kama ishara ya yeye kuwa rais mpya wa awamu ya tano.
Alisema kuwa matarajio yake katika kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuongeza yote ambayo anayasema kwenye kampeni anayaweza kutekeleza.
Alisema dhamira yake ni kuwa serikali ya viwanda ili kuinua uchumi wa watanzania na kuongeza waliochukua viwanda na wameshindwa kuviendeleza watanyang'wanywa ili wapewe wengine watakaoviendeleza.
Dk.Magufuli alisema anafahamu mambo yanayohitajika kufanywa maeneo mengi ya nchi yetu lakini kwa kuwa yupo Dar es salaam lazima azungumzie mambo yanayohusu mji huo na kuongeza mji huo lazima changamoto za msongamano umalizwe na kutatua shida ya maji.
Akizungumzia barabara za Dar es Salaam ,Dk.Magufuli Alisema kwenye awamu yake kuna barabara kadhaa ambazo zinatakiwa kujengwa kwa lami na kuongeza kuna maeneo yanatakiwa kupandishwa hadhi ili serikali ipeleke huduma muhimu kwa wananchi ambapo mabilioni ya fedha yatatumika.
Alisema ili kuondoa au kupunguza msongamano serikali ya awamu ya tano , itajenga barabara za juu katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam huku akieleza kutaanzishwa mfuko maalumu kwa ajili ya kuboresha  barabara za Jiji hilo.
Dk.Magufuli alisema barabara ya juu eneo la Tazara itaanza kujengwa kwani tayari mkandarasi amepatikana na ataanza kujenga huku huku akieleza kuwa kwake amedhamiria kumaliza msongamano uliopo kwa mipango sahihi aliyonayo.
Pamoja na yote hayo aliwaomba wananchi wa Dar es salaam kuwa wamchague awe Rais ili afanye kazi huku madereva wa nchi yetu akiahidi kuboresha maisha yao kwa kuangalia upya mikataba yao na wakati huo huo akieleza namna ambavyo atafuta ushuru kwani ni kero.
Akitumia nafasi hiyo kuwa dhamira yake ni kuboresha maisha ya wanachi na hiyo kazi anaweiza ndio maana ameiomba.
"Mawazo yangu ni kuboresha msongamano wa magari na nieleze tu nitaanzisha njia barabara ambazo zitatumia waendesha bodaboda kwani nao wanahaki ya kuongia mjini. naitwa tinga tinga sasa nipeni kura za kutosha nitinge Ikulu," alisema Dk.Magufuli.
Aliwahakikishia wakazi wa Dar es salaaam kuwa anakuwa karibu nao maana kwani ndio amelelewa na wananchi wa mkoa huo na kuongeza urais utakuwa wake na umati unaojitokeza kwenye mikutano yake inatosha kusema tu yeye ndio rais wa awamu ya tano.
Watu wazimia
Wakati huo huo eneo hilo la mkutano ambalo lilikuwa na idadi kubwa ya wananchi wapi baadhi ya wananchi walizimia kwa kukosa hewa na hiyo ilisababisha watoa huduma ya afya kuwa n jukumu la kutoka huduma.
Pia polisi walikuwa na kazi ngumu ya kidhibiti idadi ya watu waliokuwa wanataka kujinasua kwenye kundi la watu kwa kupita eneo ambalo lilikuwa na uzio .
Hata hivyo walilazimika kufungua sehemu ya uzio ili kupunguza watu waliokuwa wanakosa hewa kwa kujazana wakati wakisibiri mkutano kuanza.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya Jangwani..
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofurika kusikiliza sera na mipango ya CCM .


 Hii ndio Jangwani

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Hassan Zungu kwenye mkutano mkubwa wa kampeni Jangwani, jijini Dar es Salaam.
 Mke wa mgombea wa urais kupitia CCM Mama Janeth Magufuli akihutubia wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages