Friday, September 11, 2015

TINGA TINGA MAGUFULI ALIPOTINGISHA MUSOMA MJINI LEO

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
 Umati wa wakazi wa Musoma mjini wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli ambaye aliahidi kutatua kero ya Maji,Bara bara, Elimu na huduma za Afya.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini ambao leo walifurika kuliko kawaida kwenye uwanja wa Mkendo.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Ndugu Christopher Sanya akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma mjini kwa tiketi ya CCM Ndugu Vedastus Mathayo akihutubia kwenye mkutano wa kampeni ambao pia ulihutubiwa na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiwaelezea wakazi wa Musoma mjini uamuzi sahihi uliofanywa na CCM kumteua Mgombea wa Urais Dk. John Pombe Magufuli na kuwataka wananchi hao kumpa kura za ndio.
 Waziri Mkuu Mstaafu akihutubia wakazi wa Musoma mjini wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.

 Naibu Waziri wa  Fedha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa mji wa Musoma kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Wananchi wakifurahia hotuba za viongozi.
 Waziri wa Kilimo na Chakula na Ushirika ambaye pia ni Mgombea Ubunge jimbo la Bunda mjini Stephen Wasira akihutubia wakazi wa Musoma mjini.

 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Makongoro Nyerere akihutubia mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Dk. John Pombe Magufuli.
 Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji akifuatilia mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mhe.Mwigulu Nchemba.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Makongoro Nyerere akihutubia mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi Dk. John Pombe Magufuli.
Khadija Kopa akiwaongoza wasanii wa TOT kuburudisha kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Mkendo ,Musoma mjini.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga tumba kwenye jukwaa la TOT mara baada ya kumaliza kuhutubia.
 Emmanuel Mbasha akitumbuiza kwenye mkutano wa CCM wa kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli .
 Umati wa watu ukitawanyika.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa nyamongo ambapo aliwaambia kuwa atahakikisha makampuni ya kuchimba madini yanaweka wazi taarifa zao.


 Wakazi wa Nyamwaga Tarime wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa bango lenye ujumbe wao.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Serengeti, Tarime.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Tarime kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Rolya kwenye mkutano wa kampeni za CCM.


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.