LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 14, 2015

MKUTANO WA MAGUFULI TABORA NI ZAIDI YA MAFURIKO


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora kwenye mkutano wa kampeni za CCM
 Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitoa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa mji wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.


 Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mr. Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwakilishi wa Walemavu Ndugu Amon Anastaz Mpanju mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) akizungumza na Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega mjini Hussein Bashe na Mgombea wa Ubunge jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala (kulia) kabla ya kuhutubia wakazi wa Nzega waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Parking.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Nzega na kuwahakikishia serikali yake itajali wananchi wa kawaida kwa kuwapauhuru wa kufanya bishara,pia atahakikisha maslahi ya watumishi yanaongezwa.
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya parking Nzega kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli


Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala wakiwapa shangwe wananchi pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaji Abdallah Bulembo.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Vijijini Dk. Khamis Kigwangala akiwahutubia wananchi wa Nzega kwenye mkutano ulioongozwa na Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega mjini akihutubia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM alihutubia.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Nzega kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa kata ya Ziba wakati akiwa njiani kuelekea Nzega.
Wakazi wa Bukene wakishangilia hotuba za mgombea urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bukene
Wakazi wa Bukene wakimsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages