Sunday, September 20, 2015

MAMA SAMIA KUENDELEA NA KAMPENI MKOANI TANGA KESHO

Na Bashir Nkoromo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, inaanza kesho, Septemba 21, 2015, mkoani Tanga.

Taarifa zinasema, mkoani Tanga, Mama Samia ataanza ziara yake ya kufanya mikutano ya kampeni katika wilaya ya Mkinga, Pangani na Tanga mjini.

Kulingana a taarifa hiyo, tareehe Septemba 22, 2015, Mama Samia ataunguruma Muheza, Mlalo, Korogwe mjini, Handeni na Kilindi katika mkoa huo wa Tanga.

Baada ya mkoa wa Tanga, Mama samia ataenda mkoani Manyara wilaya ya Kiteto na baadaye mkoa wa Dodoma katika majimbo ya Nchemba na Kondoa.

Taarifa zinasema baadaye Mama samia ataenda mkoa wa Morogoro Septemba 25, 2015 katika  wilaya ya Gairo.


Baadhi ya mikoa ambayo Mama Samia amekwishafanya kampeni ni Dar es Saaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.