Monday, August 31, 2015

MAMA SAMIA AKUTANA NA MAKUNDI YA KINA MAMA MJINI DODOMA

 Mgombea Mwenza waa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda alipowasili kwenye jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, kuzungumza na kina mama wa makundi mbalimbali.
 Mama Samia akiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa wakati akienda ukumbini Kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Albaert Mgumba.
 
 Mama Samia akibishwa shuka nyeupe kuonyesha kukaribishwa kwa ukarimu na Kina mama wa Dodoma, kabla ya kuingia ukubini.
 Mama Samia akibishwa shuka nyeupe kuonyesha kukaribishwa kwa ukarimu na Kina mama wa Dodoma, kabla ya kuingia ukubini.
 Kinamama wakikoleza na kitenge kwenye shuka hiyo kumfanya Mama Samia ameremete zaidi kwa zawadi hiyo, kabla ya kuingia ukumbini
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akiwa katika picha ya pamoja na Kinamama waliompokea kwa kushirikiana  na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa (wanne kulia), kabla ya kuingia ukumbini.
 Waalikwa wote wakiwa wamesimama  ukumbini wakati Mama Samia akiingia
 Shangwe zikitawala ukumbini wakati Mama Samia akiwasili ukumbini
 Mama Samia akiwa tayari ukumbini
Mama Samia akiwa na safu ya viongozi wengine meza kuu baada ya kuwasili ukumbini
 Mama Samia akiwasalimia waalikwa kabla ya kuketi


 Shamrashamra zikiendelea ukumbini
 Waalikwa wakiwa wametulia ukumbini kuanza shughuli
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya akimkaribisha Mama samia
Mwakilishi wa kundi la wenye ulemavu akizungumza machache
 Mchumi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Dodoma, Mwanahija Abdallah akizungumza kuhusu waliovyojiandaa kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo uchaguzi mkuu wa Oktoba  mwaka huu
 Mmoja wa wajumbe waliopo katika kampeni za CCM, Ummy Mwalimu akieleza wasifu wa Mama Samia, akisema kuwa mbali ya kwamba ni mwanamke lakini Mgombea Mwenza huyo anazo sifa za ziada ambazo ni pamoja na kuwa Mwadilifu, Mchapakazi na mtu makini.
 Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Nkenge Kagera lakini akaanguka katika kura za maoni, Asupta Mshama akizungumza kuwaasa kinamama kutosusa chama wanapokosa kuchaguliwa badala yake waiunge mkono CCM iendelee kushinda uchaguzi
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma, Fatuma Mwenda akimzawadia Mama Samia kitenge
 Kisha aakamkumbatia kwa furaha
 
 Mama Tunu Pinda akizungumza mambo mbalimbali ikiwemo kuwahakikishia wenzake kwamba Mumewe Waziri Mkuu Mizengo Pinda hawezi kuhama CCM katu, na kwamba ikitokea akamaha yeye ataachana naye ili abaki CCM. Pia amewahimiza kina mama kuhakikisha wale wote waliohama CCM kwenda upinzani wanakatwa hukohuko waliko wakati wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
 Adam Kimbisa akizungumza ukumbini
 Mama Samia akiwahutubia Kina mama katika mkutano huo
 Mama Samia akiwahutubia kina mama katika mkutano huo
 Kina Mama wakimsikiliza kwa makini Mama Samia alipokuwa akiwahutubia
Kina mama wakimsikiliza kwa makini na utulivu mkubwa Mama Samia Suluhu Hassani alipokuwa akizungumza nao katika ukumbi uliopo jengo la White House Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.