Thursday, September 10, 2015

MAGUFULI ATINGA MKOANI MARA

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtoto wa Baba wa taifa ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki Makongoro Nyerere mara baada ya kuwasili mkoani Mara.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira wakati wa mapokezi mkoani Mara.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo la mkutano wa kampeni za CCM Butiama, kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na mgombea ubunge wa jimbo la Butiama Nimrod Mkono.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwaniaba ya Wazee wa Butiama.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiteta jambo na mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Nimrod Mkono.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akikimbia kuelekea jukwaani kuwasalimia wakazi wa Butiama
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere akiwasalimu wakazi wa Butiama kwenye mkutano wa kampeni za CCM,kulia ni Mbunge mwingine wa bunge hilo Mhe. Shyrose Bhanji.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji akihutubia wakazi wa Butiama kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Umati wa wakazi wa Butiama wakimsikiliza Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Butiama kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Bunda mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba Bunda.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa wasifu wa mgombea ubunge jimbo la Bunda mjini Ndugu Stephen Wasira (kushoto) na mgombea ubunge wa jimbo la Mwibala Ndugu Kange Lugola (kulia) kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Bunda mjini.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe. Stephen Wasira kwenye mkutano wa kampeni za Chama cha Mapindui uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba wilayani Bunda mkoa wa Mara.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea ubunge wa jimbo la Mwibala Ndugu kange Lugola kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Bunda mjini Ndugu Stephen Wasira.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Christopher Gachuma akihutubia wakazi wa Nyamuswa kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bunda Mjini Ndugu Stephen Wasira akihutubia wakazi wa Nyamuswa ambapo aliwataka wapinzani wasitafute sababu za kusema wameibiwa kura badala yake waweke mawakala wazuri vituoni ili wapokee vizuri majibu ya kushindwa kwao.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Nyamuswa kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia kuwa uongozi wake utakuwa wa kuchapa kazi kwa maendeleo ya Taifa.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.