Sunday, September 13, 2015

MAGUFULI ASEMA VIWANDA VITALETA MAENDELEO MAKUBWA NCHINI


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Igunga kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Barafu ambapo aliwaahidi wananchi hao kuwa ataijenga Tanzania mpya yenye viwanda na kufungua fursa za ajira.
Aliwaambia wananchi hao Tanzania ina kila kitu na kwa vile serikali zilizotangulia ziliandaa mazingira mazuri na hasa baada ya upatikanaji wa gesi nchini kutarahisisha uwekezaji kwenye viwanda na kufanya nchi iendelee kwa kasi kubwa.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Igunga kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Barafu ambapo aliwaahidi wananchi hao kuwa ataijenga Tanzania mpya yenye viwanda na kufungua fursa za ajira, akiwa amewasili kutokea mkoa wa Simiyu ambapo alifanya mikutano mbali mbali.
 Wakazi wa Igunga wakimsikiliza mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni ulioanyika kwenye viwanja vya Barafu.
 Umati wa wakazi wa Igunga ukimsikiliza mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa CCM wanaogombea katika majimbo ya Igunga na jimbo la Manonga katika mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Barafu.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa CCM wanaogombea katika majimbo ya Igunga Dk. Dalally Kafumu na jimbo la Manonga Seif Hamis Gulamali  katika mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Barafu.

  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa CCM wanaogombea katika majimbo ya Igunga na jimbo la Manonga pamoja na wabunnge wa viti maalum katika mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Barafu.
 Mgombea ubunge jimbo la Igunga Dk.Dalally Kafumu akijinadi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Barafu, Igunga.
 Mgombea ubunge jimbo la Manonga Ndugu Seif Hamis Gulamali akipika kampeni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Barafu, Igunga.
 Mbunge wa Viti maalum mkoani Tabora Mhe. Munde Tambwe akihutubia wakazi wa Igunga kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Dk. John Pombe Magufuli na kuwachagua wabunge na madiwani wa CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na wapenzi wa CCM waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbali mbali.

 Mwakilishi wa watu wenye ulemavu Ndugu Amon Mpanju akihutubia umma uliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM Igunga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Abdallah Bulembo akihutubia wakazi wa Igunga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Barafu Igunga.
 Ujumbe mzito kwenye bodaboda ya maeneo ya Malampaka .
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Malampaka wakati aliposimama kwa muda kuwasalimu akiwa njiani kuelekea Igunga.
 Wakazi wa Malampaka wakimsikiliza mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Mwigumbi wakati akiwa njiani kuelekea Igunga.
 Wakazi wa Maganzo wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Hivi ndivyo wananchi wa Maganzo walivyojitokeza kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Maganzo.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la shinyanga mjini Mhe.Stephen Masele kwa wakazi wa Kolandoto wakati akiwa njiani kuelekea Igunga. Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Kishapu ambapo aliwaeleza kuwa zao la Pamba litasaidia sana wakazi hao hasa ambapo atasimamia ujenzi wa viwanda vya nguo na nyuzi

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kishapu Ndugu Suleiman Masoud Nchambi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kishapu
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea udiwani wa Kishapu.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Igurubi akiwa njiani kuelekea Igunga ambapo ulifanyika  mkutano mkubwa wa kampeni
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.