Sunday, September 27, 2015

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI MAFINGA LEO

  • Mkutano wake waweka historia
  • Kada maarufu wa Chadema anayefahamika kwa jina la Gift Sikauka Mwachang'a ajiunga na CCM
  • Magufuli atoa somo kwa vijana kujua wapi nchi imetoka, ilipo na inapoelekea
  • Aahidi kufanya maendeleo makubwa na kuhakikisha wafanya biashara ndogo ndogo wanapewa fursa za kukuza biashara zao.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Mafinga kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika viwanja vya Wambi Mafinga ambapo aliwaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchii hii haijapiga hatua wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Mafinga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Mgombea ubunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi akihutubia wakazi wa mji huo wakati wa mkutano wa kampeni ambapo Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli alihutubia pia.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa kampeni za CCM ambao ulihutubiwa pia na mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alhaji Abdala Bulembo.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akionyesha kadi ya aliyekuwa kada wa Chadema Mafinga Gift Sikauka Mwachang'a aliyerudi CCM kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Wambi.
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akimvisha kofia ya CCM aliyekuwa  kada wa Chadema Mafinga Gift Sikauka Mwachang'a aliyerudi CCM kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Wambi.
  Gift Sikauka Mwachang'a akitangaza rasmi kukihama chama cha Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa kampeni za CCM mbele ya mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mafinga Gift Sikauka Mwachang'a akitangaza rasmi kuhama Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa kampeni za CCM mbele ya mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza mbele ya walemavu wa kusikia na kuona ambapo aliwakabidhi ilani ya uchaguzi ambayo imewazungumzia na kutaka wapewe msaada wa kuelimishwa masuala mbali mbali yalioandikwa kwenye ilani.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.