Sunday, August 9, 2015

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI UTAKAO TOA LITA MILIONI 750 LINDI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi katia\ka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

 Sehemu ya Chotea kama inavyoonekana pichani katika mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,mradi huu ukikamilika utaweza kutoa lita milioni 750 ambapo utakuwa umetosheleza mahitaji ya maji, kwa sasa wakazi wa Manispaa ya lindi wanapata lita milioni 250 na mahitaji yao ni lita milioni 500.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa mradi wa maji safi uliopo Ng'apa mkoani Lindi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali ,Wahisani na Wakandarasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Ng'apa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa mradi wa maji safi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wananchi wa kata ya Matopeni kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu.
Manispaa ya Lindi ina mpango wa kujenga  nyumba kumi (10) za gharama nafuu za walimu kwa mwaka 2015/2016.
 Wananchi wa kata ya Matopeni wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akizungumza  kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu.
Mradi huo ambao upo kwenye halmashauri 7 za mkoa wa Lindi  na ambapo katika kata ya Matopeni kwenye shule ya Msingi Mtuleni zimeanza kujengwa nyumba mbili.
 Waziri wa Ujenzi na Mgombea wa Urais kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Abdallah Ulega pamoaja na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Mtuleni mara baada ya kumaliza kukagua  mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu, Wengine pichani ni Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli, Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutokea Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakiwasalimia wananfunzi wa Shule ya Msingi Mtuleni mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu shuleni hapo.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.