Sunday, August 2, 2015

NYALANDU ASHINDA KURA ZA MAONI UBUNGE CCM SINGIDA KASKAZINI


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameibuka na ushindi wa kishindo katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania ubunge Jimbo la Singida Kaskazini.

       Nyalandu, ambaye alikitetea nafasi hiyo aliwashinda wagombea wenzake saba waliojitokeza kupambana naye, ambapo aliongoza kwenye kata zote za jimbo hilo na kuwaacha mbali wapinzani wake.

    Mwanasiasa huyo kijana na mwenye ushawishi mkubwa, aliongoza katika Kata za Ikhanoda, Msange, Itaja, Mwasauya, Mrama, Maghojoa, Ilongero, Ngimu na kuzidiwa kwa kura chache kwenye kata moja ya Mughamo.

    Matokeo ya mwisho yaliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi, yamempa ushindi Nyalandu kwa kupata kura 13,738 huku akifutiwa na Justin Monko aliyepata kura 5,648.

     Nyalandu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, anamshukuru Mungu na wanachama wa CCM jimboni humo kwa kumpa ushindi wa kishindo na wenye heshima licha ya kufanyiwa mchezo mchafu na wapinzani wake.

     Alisema wapinzani wake walicheza rafu za wazi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kuleta makundi ya watu ambao hawakuwepo kwenye orodha ya wapiga kura, kuandaa vijana wa kumzomea kwenye mikutano, lakini mwisho wa siku wananchi wameonyesha bado wana muamini na kumchagua kwa kishindo.

    “Nimekuwa kwenye siasa kwa muda sasa…lakini katika uchaguzi huu nimefanyiwa rafu nyingi sana na wapinzani wangu ila nashukuru Mungu wananchi wameonyesha bado wananiamini na imani hiyo inatokana na kazi kubwa niliyoifanya kama mbunge wao. Nitaendelea kuwatumikia kwa juhudi na akili zangu zote na kamwe sitawaangusha,” alisema Nyalandu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu  na mashabiki wake, wakishangilia baada ya Waziri huyo kutangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni ya kugombea ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja, wakishangilia na wafuasi wao baada ya Nyalandu, kutangazwa kuwa mshindi wa ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.