Tuesday, August 25, 2015

MAGUFULI AFUNGA KAZI SUMBAWANGA MJINI

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini tayari kuwahutubia wakazi wa mji huo.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa Nelson Mandela ,Sumbawanga mjini.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hilaly .
 Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya akiwahutubia wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Nelson Mandela.

 Umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM ambapo mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini hapo.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile na watendaji wazembe.
 Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hilaly akihutubia wakazi wa Sumbawanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela ambapo CCM ilikuwa ikifanya mkutano mkubwa wa kunadi sera na mikakati yake kwa wananchi.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaonyesha ishara ya ushindi wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.