LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 9, 2015

KIKWETE AZINDUA KIVUKO CHA MV. MAFANIKIO MTWARA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA NYUMBA 30 ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA SHANGANI MKOANI MTWARA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Mchemba wakati alipowasili kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Mafanikio mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana akisalimiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mtwara Nurdin Mangochi kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa kivuko cha Mv. Mafanikio mkoani Mtwara.
 Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa kivuko cha MV. Mafanikio kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Msemo feri Mtwara mjini kwenda Msanga Mkuu,Mtwara vijijini,Kivuko hicho kilichogharimu kiasi cha bilioni 3.3 na kina uwezo wa kupakia abiria 100 na mzigo wenye uzito wa tani 50.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wananchi wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia uzinduzi wa kivuko kipya cha Mv. Mafanikio.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwekajiwe la msingi kama ishara ya uzindua kivuko cha Mv.Mafanikio.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kama ishara ya kuanza kutumika kwa kivuko cha Mv.Mafanikio kitakachokuwa kinafanya safari zake kutoka Mtwara Feri kwenda Msanga Mkuu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kwenye uzinduzi wa Kivuko cha Mv. Mafanikio mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akiwa safarini kwenda kata ya Msanga Mkuu, Mtwara vijijini kwa kutumia kivuko kipya cha Mv. Mafanikio ikiwa sehemu moja ya utekelezaji wa ahadi zake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kata ya Msanga Mkuu,Mtwara vijijini.
 Kivuko cha Mv. Mafanikio
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Sheikh Nurdin Mangochi akitoa dua maalum kabla ya kuanza kwa mkutano na wananchi wa kata ya Msanga Mkuu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Marcelin Magesa akitoa taarifa fupi za kivuko cha Mv. Mafanikio kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Msanga Mkuu,Mtwara Vijijini.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego akitoa salaam za mkoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Msanga Mkuu .
 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Ghasia akizungumza kwenye mkutano huo
 Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano na wananchi wa Msanga Mkuu, Mtwara vijijini mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  kuzindua kivuko cha Mv. Mafanikio
 Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Msanga Mkuu ambao leo wamekuwa na furaha kupata kivuko cha Mv. Mafanikio ambacho kitasafirisha wanafunzi wenye sare bure pamoja na walemavu.
 Mwananchi wa Msanga Mkuu akionyesha uzalendo kwenye mkutano wa uzinduzi wa kivuko kipya cha Mv. Mafanikio.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wa Msanga Mkuu , Mtwara Vijijini mara baada ya kuzindua kivuko kipya.
 Bango la kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu akihutubia kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi wa nyumba mpya 30 zilizopo Shangani mkoani Mtwara.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Nyumba 30 za Shirika la Nyumba la Taifa zilizopo Shangani mkoani Mtwara,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Nyumba 30 za Shirika la Nyumba la Taifa zilizopo Shangani mkoani Mtwara,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu na kushoto ni Mama Salam Kikwete na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelekezo ya mchoro wa nyumba 30 za Shirika la Nyumba la Taifa zilizopo Shangani mkoani Mtwara kutoka kwa Mkurugenzi wa ujenzi wa shirika hilo Ndugu Haikaman Mlekio
 Hizi ndio sehemu ya nyumba 30 za Shirika la Nyumba la Taifa zinazojengwa Shangani mkoani Mtwara
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba 30 zilizopo Shangani mkoani Mtwara zinazojengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 4.9

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages