Monday, August 10, 2015

KIKWETE AWAAGA RASMI WANANCHI WA MTWARA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Mtwara kwenye uwanja wa Nangwanda ambapo aliwaaga wakazi hao huku akiwaambia kuwa Mtwara ndio utakuwa mji wenye uwezo wa kiuchumi Tanzania.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wakazi wa Mtwara kama ishara ya kuwaaga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona.
 Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara ambao Rais Jakaya Kikwete aliwaaga wakazi hao.
 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara ambao Rais Jakaya Kikwete aliwaaga wakazi hao
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye mkutano ambao Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaaga wakazi hao , Sinani alisema Jakaya amewafanyia mengi mazuri wakazi wa Mtwara na kumshukuru kwa kuiongoza nchi kwa miaka 10.

 Mbunge wa Mtwara Mjini Hasnain Murji akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara ambao Rais Jakaya Kikwete aliwaaga wakazi hao kwani hatopata nafasi ya kurudi tena akiwa kama Rais na badala yake akija atakuwa Mwananchi Maarufu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Nahemia Mchechu akihutubia wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara ambao Rais Jakaya Kikwete aliwaaga wakazi hao
 Mzee Yusuph akitumbuiza wakazi wa Mtwara
 Kikundi cha ngoma kikionyesha uwezo wa kucheza Sindimba
Wasanii wa Mtwara All Stars wakitumbuiza kwenye mkutano ambao Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaaga rasmi wakazi wa mkoa wa Mtwara.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.