Saturday, August 8, 2015

KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU - SOMANGA YENYE UREFU WA KILOMITA 60

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.
 Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua barabara yenye urefu wa kilomita 60 ya Ndundu mpaka Somanga.
Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.

 Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda kwenye ufunguzi wa bara bara ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 60 ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ,Jassem Ibrahim Al Najem akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.
 Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.
 Helkopta iliyombeba Mheshimiwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa imetua kwenye barabara ya lami ya Ndundu-Somanga kwenye kijiji cha Marendego sehemu ambapo sherehe za ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga ulifanyika.
 Wananchi wakiwa wamejipanga kushuhudia ufunguzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 60 ya Ndundu mpaka Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakishangilia kukamilika kwa ujenzi sehemu korofi ya barabara inayounganisha Dar es salaam, pwani na mikoa ya Lind na Mtwara, barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, iliyojengwa kwa kiwango cha Lami.


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.