Sunday, August 9, 2015

JK AKEMEA DHULMA KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye kilele cha sherehe za nane nane mkoani Lindi ambapo alizungumzia kukua kwa sekta ya kilimo na matumizi mazuri ya matrekata pamoaja na mbolea, pia kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwani itawasaidia sana wakulima lakini pia alikemea vitendo vya dhulma vinavyofanya na vyama vya ushirika kwa wakulima.
Rais Dkt. Jakaya alitumia fursa hiyo kuwaaga wakazi wa mkoa wa Lindi
 
 Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumzia miradi ya barabara iliyokamilika  mpaka sasa na iliyokuwa kwenye utaratibu wa kukamilishwa wakati wa kufunga sherehe za nane nane mkoani Lindi.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Uusiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza masuala ya usalama wa mipaka yetu pamoja na mahusiano na nchi jirani kwenye kilele cha siku ya nane nane iliyofanyika Kitaifa mkoani Lindi.

 Vyombo vya habari vilikuwa vingi kuchukua matukio kwenye siku ya kilele cha sherehe za wakulima nane nane.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kombe kwa mmoja wa washiriki wa Nane nane mkoani Lindi.
 Washindi wa jumla JKT wakiwa kwenye picha ya pamoja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza tufe kuashiria kufunguliwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwenye kilele cha sherehe za Nane Nane mkoani Lindi.

Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.