Sunday, August 16, 2015

JK AFUNGUA BARAZA LA VIJANA WA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa NEC Jerry Slaa
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye Baraza la Vijana wa CCM
 Wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Wajumbe wa Baraza la Vijana wakiwa kwenye hamasa ya hali ya juu.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda akihutubia Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM
 Wageni waalikwa kutoka nje ya Nchi (Diaspora)
 Dk.Emmanuel Nchimbi akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM
 Mgombea Urais kwa tiketi ya |CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM na kuwaambia kuwa atashirikiana nao vizuri.
 Wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.


 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Sixtus Mapunda wakihimiza vijana kuwa imara.
 Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Vijana wa CCM
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiteta jambo na Dk. Emmanuel Nchimbi.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa NEC Vijana mara baada ya kufungua na kumaliza kuhutubia Baraza la Vijana wa CCM.


TAMKO LA BARAZA LA VIJANA WA CCM
Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International convention centre, pamoja na mambo mengine liliazimia mambo yafutauo:-
1. Lilimvua Ukamanda Mkuu ndugu Kingunge Ngombale Mwiru. Maamuzi hayo yalitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kuenda tofauti na maadili na taratibu za CCM.
Aidha kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
2. Kikao pia kiliunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.
3. Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.

Sixtus Raphael Mapunda
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa

 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.