Friday, July 31, 2015

NYALANDU AJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA SINGIDA KASKAZINI

Na Mwandishi wetu
KATIBU CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku, amesema mchakato wa kampeni kwa wagombea wanaowania ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini, unaendelea vizuri.

Pia, amesema changamoto zilizojitokeza ikiwemo baadhi ya wagombea kulalamika kufanyiwa rafu, yamepatiwa na yataendelea kupatiwa ufumbuzi kwa njia halali za vikao.

Aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kufanya kikao na wagombea wanaowania ubunge kwenye jimbo hilo, ambalo linaongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Jana, Mary alifanya kikao na wagombea hao ambapo masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo malalamiko miongoni mwa wagombea.

Jimbo hilo mbali na Nyalandu, pia linawaniwa na Amos Makiya, Justin Monko, Michael Mpombo, Sabasaba Manase, Yohana Sintoo, Mungwe Athumani na Aron Mbogho.

Katika mkutano huo ambao uliisha kwa wagombea wote kuunga na kutaka kufanyike kampeni za kistaarabu.

Awali, Mary alisema kuwa baadhi ya wagombea walikuwa wakilalamika kuchezewa rafu, ambapo baadhi walimlalamikia Nyalandu, ambaye pia aliwalalamikia wagombea wenzake kufanya kampeni chafu dhidi yake ikiwemo kuandaa watu kumzomea kwenye mikutano.

“Kulikuwa na malalamiko miongoni mwa wagombea na ndio sababu tumeitana hapa ili kuzungumza ili kufikia mwafaka na kuendelea na kampeni. Kila mmoja amezunguza na ni mambo madogo ambayo hayana madhara katika mchakato,” alisema Mary na kuongeza kuwa: Nyalandu alilalamika wenzake kuandaa vijana wa kumzomea kwenye mikutano ili ashindwe kujieleza, jambo ambalo tumelizungumza pia.

“Baada ya kupitia malalamiko hayo na mengine mengi kwa pamoja tumekubaliana yote hayo yanatokana na joto kali la uchaguzi wa mwaka huu na hayajavunja kanuni zetu”.

Mary alisema kuwa wagombea wote wamekubaliana kuwa malalamiko hayo yamekwisha na wanasonga mbele na kampeni kwa ajili ya kuomba ridhaa ya wana-CCM na kukitanguliza Chama kwanza katika kila kitu.

Alipoulizwa na waandishi wa habari, Nyalandu alisema malalamiko yaliyotolewa na wagombea wenzake ni dalili za kuashiria kushindwa.

Alisema miaka yote amekuwa akiendesha kampeni za kistaarabu ndani na nje ya Chama na kwamba, anatambua kanuni na taratibu za CCM.

“Nitumie fursa hii kuwaasa wanasiasa wenzangu kuacha vitendo vya rushwa, kupakana matoke, uzushi na uongo uliopitiliza. Tufanye siasa safi kwa maslahi ya wapigakura wetu na CCM kwa sababu kununua watu ili wanizomee bila sababu ya msingi ni kosa.

“Najivunia kazi kubwa niliyoifanya kwa wananchi wangu na jimbo langu na ndio sababu ninasimama tena kuomba ridhaa ya wananchi ili niendelee kuwatumikia,” alisema Nyalandu.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.