Friday, July 24, 2015

MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI WA TANZANIA AONGOZA KIKAO CHA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA

 Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Bodi ya  Ukaguzi ya  Umoja wa  Mataifa, Bw.Mussa Juma Assad akizungumza wakati wa hitimisho la mkutano wa siku mbili wa Bodi hiyo uliofanyika hapa Umoja wa Mataifa kuanzia Julai 22-23. Kushoto kwake ni Bw. Fransis Kitauli,  Mkurugenzi wa Ukauzi wa Nje  na  Mwenyekiti wa  Kamati ya  Operesheni za Ukaguzi ( AOC) Akiwa Mwenyekiti wa   AOC Bw. Kitauli ambaye alishika nafasi  hiyo tangu mwaka 2012 amefanikisha  utoaji wa ripoti za ukaguzi za Umoja wa Mataifa kwa  miaka mitatu mfululizo
 Wajumbe wa  Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa  Serikali ya India,  Bw. Shashi Kant Sharma,  Sir Amyas Morse,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya India na Bw. Mussa Juma Assad,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Tanzania wakitia saini zao katika  ripoti 28 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa siku mbili. ripoti hizo ni  matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.