Monday, June 8, 2015

ZIARA YA KINANA YAONGEZA MATUMAINI KWA WANANCHI MULEBA, AWATAKA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SHUGHULI ZAO

*AWAFAGILIA WABUNGE MWIJAGE NA PROFESA ANNA TIBAIJUKA
*ASEMA WAMEFANYA MAKUBWA KATIKA MAJIMBO YAO
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amezungukwa na umati wa wananchi, alipohutubia mkutano wa hadhara, leo katika mji mdogo wa Nshamba, jimbo la Muleba Kusini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika mkoa wa Kagera
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia umati huo wa wananchi katika mutano huo wa Kinana uliofanyika leo katika mji mdogo wa Nshamba, wilayani Muleba
 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akihutubia mkutano huo wa hadhara wa Kinana, uliofanyika leo katika mji mdogo wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera
 Baadhi ya wananchi waliokuwa pembezoni, nao wakifuatilia kwa makini kila kilichokuwa kikijiri kwenye mkutano wa Kinana uliofanyika leo katika mji mdogo wa Mshamba.
 Katibu Mkuu wa CCM, akipokea zawadi ya muwa aliopewa na wananchi baada ya kuhutubia mutano wa hadhara uliofanyika leo katika mji mdogo wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na zawadi zilizofungwa kiasili, ambazo alikabidhiwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji huo mdogo wa Nshamba. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Wananchi wakiwa wamelizonga gari kwa shauku ya kutaka kusalimiana na a Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera
 Katibu Mkuuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu, jengo la Ofisi ya CCM, Wilaya ya Muleba, baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo ambao unaendelea, leo.
 Ofisi hiyo ya CCM wilayani Muleba ambayo ujenzi wake unaendelea
 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akisaidia kupiga lipu jengo hilo, Katibu Mkuu wa CCM alipofika kukagua ujenzi wa jengo la Ofii hiyo ya CCM leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahma Kinana akiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM wilaya ya Muleba leo. Kushoto ni Kada wa CCM, Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (kulia) wakati akitoa maelezo kuhusu ukarabati mkubwa uliofanyika kuufufua mradi wa maji wa Nshamba, wilayani Muleba mkoani Kagera, leo. Alisema, mradi huo ambao ulikufa zaidi ya miaka 30 iliyopita, umeweza kufufuka kwa juhudi zake za kutafuta msaada wa fedha  kutoka Umoja wa Mataifa.
 Msimamizi wa mradu huo wa maji akimpatia Kinana maelezo kuhusu mradi huo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitazama hatua iliyofikiwa katika kuufufua mradi huo wa maji
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Nshamba, alipotembea mradi wao wa maji leo Kinana amewataka wananchi hao kuhakikisha katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu wanachagua viongozi ambao wanasimamia miradi kwa faida ya wananchi na siyo kuchagua wanatafuta kunufaisha matumbo hiyo, na kwamba moja ya njia ya kufanikisha kupata viongozi wazuri ni kuchagua watu wenye shughuli zao.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionyeshwa ukarabati mkubwa uliofanyika kwenye eneo la kuhifadhia maji, kwenye mradi huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungulia maji, kujaribu kama mradi huo umefikia hatia nzuri ya kuweza kuhudumia wananchi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abulrahman Kinana akitoka kukagua mradi huo wa maji
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa na Mwenyekiti wa zamani wa CCM wilaya ya Muleba, Simon Katarama aliyefika kuwasalimia wakati wakikagua mradi wa Maji wa Nshamba, leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua chumba cha kompyuta kaika shule ya sekondari ya Nyakatanga, wilayani Muleba mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuhusu mradi huo wa kompyuta kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia masomo ya sayansi katika shule hiyo. Kompyuta hizo zimetolewa na Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage (kushoto).
 Kompyuta zilizomo kwenye chumba hicho cha masomo ya sayansi
 Katibu Mkuu wa CCM na baadhi ya viongozi wakishirikiana na baadhi ya wananchi kuvuta waya wa meme, kusaidia katika utandazaji nyaya katika mradi wa umeme unaofanyika Nyakatanga, wilayani Muleba mkoa wa Kagera, Kinana alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa huo, leo
 Wananchi wa kijiji cha Mushabango wilayani Muleba mkoani Kagera, wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili katika kijiji hicho kuhutubia mkutano wa hadhara, leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara aliofanya katika kijiji cha Mushabango wilayani Muleba mkoani Kagera leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akiwapa vidonge vyao wapinzani alipohutubia mkutano huo wa Kinana katika Kijiji cha Mushabngo, wilayani Muleba mkoani Kagera. Amesema katika uchaguzi mkuu ujao, CCM itaibuka na ushindi wa kishindo na kuwaacha wapinzani hao 'wakisoma namba kwa mbaaaali"
 Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akiwahutubia wananchi katika mkutano huo wa Mushabango
 Wananchi wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM alipowasili katika Kijiji cha Kamachumu wilayani Muleba  kuhutubia mkutano wa hadhara
  
 Kinana akishiriki kucheza ngoma za asili alipopokewa kwa ngoma, katika Kijiji cha Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera
  Kinana akishiriki kucheza ngoma za asili alipopokewa kwa ngoma, katika Kijiji cha Kamachumu wilayani Muleba mkoani Kagera
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kamachumu, wilayani Muleba mkoani Kagera leo.
 Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kamachumu wilayani Muleba mkoani kagera
 Mzee Abdulrajabu akimzawadia Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, baada ya kuhutubia wananchi katika kijiji cha Muleba mkoani Kagera, leo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana akikabidhi basikeli kwa ajili ya Makatibu wa CCM kata zilizopo jimbo la Muleba Kaskazini, baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa jimbo hilo Charles Mwijage (kulia)
 Katibu Mkuu wa CCM akikabidhiwa na Mbunge wa Muleba Kaskazini, mipira ya maji kwa ajili ya kina mama wanaofanya kilimo cha umwagiliaji.
 Katibu Mkuu wa CCM akikabidhi majembe kwa Kina mama wakulima katika kijiji cha Kamachumu, baada ya kuhutubia mkutano huo. majembe hayo pia yametolewa na Mbunge Mwijage
 Wamasai wanaoishi katika Kijiji cha Kamachumu, wilayani Muleba mkoa wa Kagera wakifuatilia mambo yalivyokuwa yakienda katika mkutano wa Kinana uliofanyika katika kijiji hicho cha Muleba leo

 Vijana wanaofanyakazi katika mradi wa mabwawa ya kufugia samaki wa Ruhanga, katika Kijiji cha Izigo mkoani Kagera, wakiwa kazini leo
 Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage akimpa maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu mradi wa mabwawa ya ufugaji samaki, alipokagua mradu huo leo.
 Katibu Mkuu wa CCM akitazama eneo la kukuzia samaki wa awali
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Profesa Anna Tibaijuka wakitazama vinapofugiwa 'vifaranga' vya samaki kabla ya kuwekwa kwenye mabwawa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mradi huo.
 Katibu Mkuu wa CC, Abdulrahman Kinana akinawa maji baada ya kukagua mradi huo wa samaki
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Izigo, wilayani Muleba mkoani Kagera leo
 Wananchi wa Izigo wakimshangilia Kinana kwenye mkutano huo
 Naam kila mmoja akimshangilia Kinana kwenye mkutano huo
 Mbunge, Mwijage akishiriki kusakata ngoma za kienyeji na wananchi wa jimbo lake kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amezungukwa na mamia ya wananchi kwenye mkutano huo wa Izigo, wilayani Muleba

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha zigo
 Wananchi wa Izigo wakimshangilia Kinana katika mkutano huo
 Kinana akisistiza jambo alipowahutubia wananchi katika mkutano huo wa Izigo
 Kijana kutoka Chadema, akizungumza mbele ya Nape baada ya kutangaza kuhamia CCM
 Kinana akikabidhi baiskeli kwa makatibu wa CCM wa Kata za jimbo la Muleba Kaskazini baada ya mkutano huo wa Izigo
 Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa muleba Kaskazini, Mwijage wakiteta jambo wakati wa mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika Izigo, leo
"ETI HUYU KIJANA HUYU WA CHADEMA, NDIYO ANATAKA KUPAMBANA NA CCM KATIKA UCHAGUZI MKUU, HAPA MULEBA" inaelekea ndivyo alivyokuwa akisema, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kulia) wakati akimtambulisha kwa Kinana, Mhariri wa zamani wa Tanzania Daima Asbert Ngurumo, ambaye alifika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu huyo wa CCM  uliofanyika leo katika kijiji cha Zigo, wilayani Muleba. Picha zote na Bashir Nkoromo)
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.